// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA YAAMBULIA SARE KWA KVZ MECHI YA MWISHO MAPINDUZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA YAAMBULIA SARE KWA KVZ MECHI YA MWISHO MAPINDUZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Thursday, January 04, 2024

  YANGA YAAMBULIA SARE KWA KVZ MECHI YA MWISHO MAPINDUZI


  TIMU ya Yanga SC imekamilisha mechi zake za Kundi C Kombe la Mapinduzi kwa sare ya bila mabao na KVZ usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Yanga inamaliza mechi zake za Kundi hilo na pointi saba, ikifuatiwa na KVZ pointi tano na zote zimefuzu Robo Fainali, wakati Jamus FC ya Sudan Kusini ina pointi moja nafasi ya tatu na Jamhuri ambayo haina pointi inashika mkia.
  Ni Jamhuri na Vital’O zitakazohitimisha mechi za Kundi hilo kwa kumenyana kesho.
  Timu mbili za juu katika makundi A, B na C zitafuzu moja kwa moja Robo Fainali wataungana na washindi wa tatu bora wawili wa makundi hayo kukamilisha timu nane za kuwania Nusu Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAAMBULIA SARE KWA KVZ MECHI YA MWISHO MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top