• HABARI MPYA

  Thursday, January 25, 2024

  LIVERPOOL YATINGA FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND


  TIMU ya Liverpool FC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup licha ya sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Fulham jana Uwanja wa Craven Cottage Jijini London.
  Mshambuliaji Mcolombia, Luis Díaz alianza kuifungia Liverpool dakika ya 11, kabla ya beki Mfaransa, Issa Diop kuisawazishia Fulham dakika ya 76.
  Liverpool inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 kufuatia ushindi wa nyumbani wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Januari 10 Uwanja wa Anfield.
  Na sasa Liverpool itamenyana na Jumapili ya Februari 25 kuanzia Saa 1:30 usiku Uwanja wa Wembley Stadium Jijini London.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YATINGA FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top