• HABARI MPYA

  Sunday, January 14, 2024

  IVORY COAST YAANZA VYEMA AFCON, YAICHAPA GUINEA-BISSAU 2-0


  WENYEJI, Ivory Coast usiku wa jana walianza vyema kampeni yao ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuichapa Guinea-Bissau mabao 2-0 katika mechi ya ufunguzi ya Kundi A Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara Jijini Abidjan.
  Mabao ya Ivory Coast jana yalifungwa na kiungo wa Al Nassr ya Saudi Arabia, Seko Mohamed Fofana dakika ya nne na mshambuliaji wa Red Star Belgrade ya Serbia, Jean-Philippe Nil Stephan Krasso dakika ya 58.
  Mchezo mwingine ya Kundi A utafuatia leo baina ya Nigeria ‘Tai Mkubwa’ na Equatorial Guinea ‘Radi ya Taifa’ Saa 11:00 jioni hapo hapo Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara Jijini Abidjan.

   

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IVORY COAST YAANZA VYEMA AFCON, YAICHAPA GUINEA-BISSAU 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top