• HABARI MPYA

  Tuesday, January 09, 2024

  MLANDEGE YATINGA FAINALI KWA MATUTA KOMBE LA MAPINDUZI


  MABINGWA watetezi, Mlandege SC wamefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa penalti 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Shujaa wa Mlandege leo kwa mara nyingine amekuwa kipa wake Othman Hassan aliyeokoa penalti mbili za wachezaji wa APR, Sharaf Shiboub na Ramadhan Niyibizi, huku za Eric Ndayishimiye na Soulei Sanda pekee zikimpita.
  Waliofunga penalti za Mlandege ni Mjamaica Malik Zidan, Emanuel Pius, Said Mussa Said na Mganda Arafat Galiwango, huku mkwaju wa Yussuf Suleiman Hajji ‘Jusa’ ukiokolewa na kipa Pierre Ishimwe wa APR.
  Sasa Mlandege itasubiri kukutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kesho baina ya Simba SC na Singida Fountain Gate hapo hapo New Amaan Complex.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MLANDEGE YATINGA FAINALI KWA MATUTA KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top