• HABARI MPYA

  Tuesday, January 30, 2024

  IVORY COAST YAIVUA SENAGAL UBINGWA KWA MATUTA


  TIMU ya Senegal imevuliwa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kufungwa kwa penalti 5-4 na wenyeji, Ivory Coast katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro mjini Yamoussoukro.
  Mshambuliaji wa Al Shabab, Mouhamadou Habibou Diallo alianza kuifungia Senegal dakika ya nne tu akimalizia krosi ya mkongwe, Sadio Mané wa Al Nassr kabla ya Franck Kessié wa Al Ahli, zote za Saudí Arabia kuisawazishia Ivory Coast kwa penalti dakika ya 86.
  Sasa Ivory Coast itakutana na Cape Verde katika Robi Fainali ambayo iliitoa Mauritania kwa kuichapa 1-0 katika mchezo uliotangulia jana, bao pekee la  Ryan Mendes kwa penalti dakika ya 88 Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IVORY COAST YAIVUA SENAGAL UBINGWA KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top