// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SALAH APIGA MBILI LIVERPOOL YAIKANDA NEWCASTLE 4-2 ANFIELD - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SALAH APIGA MBILI LIVERPOOL YAIKANDA NEWCASTLE 4-2 ANFIELD - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Tuesday, January 02, 2024

  SALAH APIGA MBILI LIVERPOOL YAIKANDA NEWCASTLE 4-2 ANFIELD


  TIMU ya Liverpool imeuanza vyema mwaka 2024 baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Misri, Mohamed Salah mawili, dakika ya 49 akimalizia pasi ya Darwin Núñez na la penalti dakika ya 86, mengine kiungo Muingereza Curtis Jones dakika ya 74 na mshambuliaji Mholanzi Cody Gakpo dakika ya 78.
  Kwa upande wao Newcastle United mabao yao yamefungwa na mshambuliaji Msweden mwenye asili ya Eritrea, Alexander Isak dakika ya 54 na beki Mholanzi, Sven Botman dakika ya 81.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 45 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tatu zaidi ya Aston Villa baada ya wote kucheza mechi 20, wakati Newcastle United inabaki na pointi zake 29 za mechi 20 pia nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH APIGA MBILI LIVERPOOL YAIKANDA NEWCASTLE 4-2 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top