• HABARI MPYA

  Sunday, January 07, 2024

  MAN CITY YAICHAPA HUDDERSFIELD 5-0 ETIHAD


  TIMU ya Manchester City imefanikiwa kutinga Raundi ya Nne ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Huddersfield Town leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.

  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Phil Foden mawili dakika ya 33 na 65, Julian Alvarez dakika ya 37, Ben Jackson aliyejifunga dakika ya 58 na Jeremy Doku dakika ya 74.  
  Kocha Mspaniola , Pep Guardiola leo alimuanzisha kiungo wake Mbelgiji, Kevin de Bruyne kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje kwa takriban miezi mitano tangu Agosti mwaka jana kutokana na maumivu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAICHAPA HUDDERSFIELD 5-0 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top