ROBO za Kombe la Mapinduzi 2024 zitaanza Jumapili kwa mabingwa watetezi, Mlandege SC kumenyana na KVZ Saa 10:15 jioni Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
Robo Fainali ya pili itafuatia Jumapili Saa 2:15 kati ya Yanga SC na APR ya Rwanda hapo hapo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
Jumatatu Saa 10:15 jioni Azam FC itamenyana na Singida Fountain Gate, kabla ya Simba SC kucheza na Jamhuri SC Saa 2:15 usiku hapo hapo New Amaan Complex.
0 comments:
Post a Comment