• HABARI MPYA

  Monday, January 01, 2024

  YANGA SC YAANZA NA MOTO KOMBE LA MAPINDUZI, YASHINDA 5-0


  MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC jana wameanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Jamhuri katika mchezo wa Kundi C Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
  Mabao ya Yanga SC yalifungwa na mshambuliaji Crspin Ngushi mawili dakika ya 10 na 17, beki Kibwana Shomari dakika ya 17, mshambuliaji Clement Mzize dakika ya 36 na kiungo wa Afrika Kusini, Mahlatse Manoka 'Skudu' Makudubela dakika ya 45.
  Mchezo uliotangulia wa Kundi C, KVZ ilitoa sare ya kufunganabao 1-1 na Jamus FC ya Sudan Kusini hapo hapo Uwanja wa New Amaan Complex.
  Yusif Mursal alianza kuwafungia Jamus dakika ya 45 kwa penalti, kabla ya Yussuf Mfaume dakika ya 64.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAANZA NA MOTO KOMBE LA MAPINDUZI, YASHINDA 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top