• HABARI MPYA

  Monday, January 08, 2024

  AZAM FC YATUPWA NJE YA KOMBE LA MAPINDUZI


  TIMU ya Azam FC imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Singida Fountain Gate katika mchezo wa Robó Fainali leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Mabao ya Singida Fountain Gate yamefungwa na washambuliaji Mkenya, Elvis Rupia dakika ya 62 na mzawa, Habib Kyombo dakika ya 65 baada ya mshambuliaji Msenegal, Alassane Diao kuanza kuifungia Azam FC dakika ya 45 na ushei.
  Sasa Singida Fountain Gate itakutana na mshindi wa Robó Fainali ya mwisho katí ya Simba SC na Jamhuri zitakazomenyana Saa 2:15 usiku huu hapo hapo New Amaan Complex.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YATUPWA NJE YA KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top