• HABARI MPYA

  Tuesday, January 02, 2024

  AZAM FC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI


  TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Robó Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Vital’O ya Burundi leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na mshambuliaji Msenegal, Alassane Diao mawili dakika ya tisa na 57 na beki Pascal Gaudence Msindo dakika ya 72, wakati bao pekee la Vital’O limefungwa na Jean Nzeyimana kwa penalti dakika ya 63.
  Azam FC inakamilisha mechi zake za Kundi A na pointi saba baada ya sare ya 0-0 na mabingwa na watetezi, Mlandege na ushindi wa 1-0 dhidi ya Chipukizi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top