• HABARI MPYA

  Monday, January 15, 2024

  CAPE VERDE YAIDUWAZA GHANA, NIGERIA NA MISRI ZATOA SARE

   

  BAO la dakika ya 90 na ushei la winga wa Ankaragücü ya Uturuki, Garry Mendes Rodrigues liliiwezesha Cape Verde kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Ghana katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mataifa ya Afrika jana Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan. 
  Cape Verde ilitangulia kwa bao la dakika ya 17 la kiungo waSan Jose Earthquakes ya California, Marekani Jamiro Gregory Monteiro Alvarenga, kabla ya Alexander Djiku kuisawazishia Ghana dakika ya 56.
  Mechi nyingine ya Kundi B jana, Misri ilitoa sare ya 2-2 na Msumbiji hapo hapo Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny, mabao ya Mamba yakifungwa na mawinga, Witiness Chimoio João Quembo 'Witi'  wa Nacional ya Ureno na Clésio Palmirim David Baúque wa Gabala ya Azerbaijani. 
  Sasa Cape Verde inaongoza Kundi B kwa pointi zake tatu, ikifuatiwa na Misri na Msumbiji zenye pointi moja kila moja, wakati Ghana inaanzia nyuma ya timu zote hizo.
  Mapema jana ulipigwa mchezo wa Kundi A Nigeria ikilazimisha sare ya 1-1 na Equatorial Guinea, 
  Radi ya Taifa wakitangulia kwa bao la mshambuliaji wa Ceuta anayecheza kwa mkopo Miedź Legnica, Iván 'Iban' Salvador Edú dakika ya 36, kabla ya Victor James Osimhen kuwasawazishia Tai dakika ya 38.
  Wenyeji, Ivory Coast ndio wanaongoza Kundi A baada ya kuifunga Guinea-Bissau 2-0 kwenye mchezo wa ufunguzi Jumamosi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAPE VERDE YAIDUWAZA GHANA, NIGERIA NA MISRI ZATOA SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top