• HABARI MPYA

  Wednesday, January 31, 2024

  ARSENAL YAICHAPA NOTTINGHAM FOREST 2-1 THE CITY GROUND


  TIMU ya Arsenal jana imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England 
  Uwanja wa The City Ground mjini Nottingham, Nottinghamshire.
  Mabao ya Arsenal yalifungwa na Gabriel Jesus dakika ya 65 na Bukayo Saka dakika ya 72, wakati bao pekee la Nottingham Forest lilifungwa na Taiwo Awoniyi dakika ya 89.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 46 katika mchezo wa 22 na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na Liverpool ambayo pia ina mechi moja mkononi, wakati mabingwa watetezi, Manchester City wana pointi 43 za mechi 20 nafasi ya tatu.
  Nottingham Forest baada ya adhabu hiyo wanabaki na pointi zao 20 za mechi 22 nafasi ya 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA NOTTINGHAM FOREST 2-1 THE CITY GROUND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top