• HABARI MPYA

  Friday, January 26, 2024

  TANZANIA NA IVORY COAST ZATAKA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA MICHEZO


  WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Michezo wa Ivory Coast, Adjé Silas na kujadili juu ya kusaini makubaliano maalum ya ushirikiano (MOU) katika sekta ya michezo baina ya nchi hizo ili kuibua na kukuza vipaji.
  Waziri Ndumbaro ameipongeza nchi hiyo kwa maandalizi mazuri ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yanayoendelea kwa kujenga miundombinu mizuri ikiwemo viwanja na barabara
  Amesema Tanzania inajifunza kwa Ivory Coast kwa kuwa itakua mwenyeji wa michuano hiyo kwa kushirikiana na Kenya na Uganda mwaka 2027
  Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi wa Michezo kutoka Tanzania, Ally Mayai na viongozi wengine wa Wizara ya Michezo wa Ivory Coast.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA NA IVORY COAST ZATAKA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA MICHEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top