• HABARI MPYA

  Tuesday, January 16, 2024

  SENEGAL YAANZA NA MOTO, CAMEROON NA ALGERIA DROO


  MABINGWA watetezi, Senegal jana wameanza vyema kampeni ya kulinda taji lao kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya  Gambia katika mchezo wa Kundi C Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika uliofanyika Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro mjini Yamoussoukro, Ivory Coast.
  Mabao ya Simba wa Teranga yalifungwa na viungo, Pape Alassane Gueye wa Marseille dakika ya nne na Mamadou Lamine Camara wa Metz, zote za Ufaransa mawili dakika ya 52 na 86.
  Mechi nyingine ya Kundi C jana,
  Cameroon ilitoka sare ya 1-1 na Guinea hapo hapo Charles Konan Banny de Yamoussoukro.
  Mabao yote yalifungwa na nyota wanaocheza Ufaransa, Mohamed Lamine Bayo wa Le Havre, akianza kuifungia Guinea dakika ya 10, kabla ya Frank Mario Magri wa Toulouse kuisawazishia Cameroon dakika ya 51.
  Senegal inaanzia kileleni mwa Kundi C kwa pointi zake tatu ikifuatiwa na Cameroon na Guinea zenye pointi moja kila moja, wakati Gambia ambayo haina pointi inashika mkia.
  Mechi ya mwisho jana ilikuwa ya Kundi D baina ya Algeria na Angola ambayo ilimalizika kwa sare ya 1-1 Uwanja wa Bouaké.
  Mshambuliaji wa Al-Sadd ya Qatar, Baghdad Bounedjah alianza kuifungia Algeria dakika ya mshambuliaji wa Al Ittihad ya Misri, Agostinho Cristóvão Paciência kuisawazishia Angola dakika ya 68 kwa penalti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SENEGAL YAANZA NA MOTO, CAMEROON NA ALGERIA DROO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top