• HABARI MPYA

  Thursday, January 04, 2024

  SARE ZAIPELEKA MLANDEGE ROBÓ FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI


  MABINGWA watetezi, Mlandege SC wamekamilisha mechi zao za Kundi A Kombe la Mapinduzi kwa sare ya kufungana bao 1-1 na Chipukizi United leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Mshambuliaji Mjamaica, Khori Bennett alianza kuifungia Mlandege SC dakika ya 16, kabla ya Mundhir Mohamed kuisawazishia Chipukizi United dakika ya 25 kwa penalti.
  Kwa matokeo hayo, Mlandege inamaliza na pointi tatu baada ya sare katika mechi zao zote na wanaungana na Azam FC iliyomaliza na pointi saba kwenda Robó Fainali ya michuano hiyo, wakati Chipukizi inamaliza nafasi ya tatu na pointi zake mbili, ikiiIdi tu wastani wa mabao Vital’O ya Burundi iliyoshika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SARE ZAIPELEKA MLANDEGE ROBÓ FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top