• HABARI MPYA

  Wednesday, January 10, 2024

  CHELSEA YACHAPWA 1-0 NA MIDDLESBROUGH KOMBE LA LIGI ENGLAND


  WENYEJI, Middlesbrough wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chelsea usiku wa jana katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup Uwanja wa Riverside mjini Middlesbrough.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Hayden Hackney dakika ya 37 na sasa timu hizo zitarudiana Januari 23 Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London na mshindi wa jumla atakwenda Fainali ya michuano hiyo.
  Nusu Fainali nyingine ya Carabao Cup ni leo kati ya Liverpool na Fulham Uwanja wa Anfield kabla ya timu hizo kurudiana Januari 24 Uwanja wa Craven Cottage Jijini London.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YACHAPWA 1-0 NA MIDDLESBROUGH KOMBE LA LIGI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top