• HABARI MPYA

  Saturday, January 06, 2024

  SIMBA SC YASAJILI KIUNGO MLINZI MSENEGAL ALIYEKUWA ANAKIPIGA TUNISIA


  KLABU ya Simba imemsajili kiungo wa ulinzi, Msenegal, Babacar Sarr kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake US Monastir ya Tunisia.
  Sare aliibukia klabu ya Wallydann, kabla ya kuhamia AS Pikine mwaka 2015, baadaye Mbour P.C. mwaka 2017, kabla ya kurejea AS Pikine mwaka 2018 zote za kwao, Senegal.
  Mwaka 2019 alijiunga na klabu maarufu Senegal, Teungueth FC ambako alicheza hadi mwaka 2021 akahamia Tunisia alikoanza na Olympique Beja hadi mwaka jana alipohamia 2023 US Monastir na sasa anatua ‘Unyamani’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASAJILI KIUNGO MLINZI MSENEGAL ALIYEKUWA ANAKIPIGA TUNISIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top