• HABARI MPYA

  Sunday, April 09, 2023

  DODOMA JIJI YATOA SARE 1-1 COASTAL UNION


  TIMU za Dodoma Jiji FC na Coastal Union zimegawana pointi kwa sare ya kufungana bao 1-1 leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Maabad Maulid alianza kuwafungia Coastal Union dakika ya 49, kabla ya Raizin Hafidh kuwasawazishia wenyeji, Dodoma Jiji dakika ya 87 akiifunga timu yake ya zamani.
  Kwa matokeo hayo, Dodoma Jiji inafikisha pointi 28 na kusogea nafasi ya 10, wakati Coastal Union inafikisha pointi 27 na kusogea nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi 26.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YATOA SARE 1-1 COASTAL UNION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top