• HABARI MPYA

  Thursday, April 13, 2023

  REAL MADRID YAICHAPA CHELSEA 2-0, AC MILAN 1-0 NAPOLI


  MABINGWA watetezi, Real Madrid wametanguliza mguu moja Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Chelsea kwenye Robo Fainali ya kwanza usiku wa Jumatano Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid.
  Katika mchezo huo ambao Chelsea ilimaliza pungufu baada ya Ben Chilwell kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 59 kwa kumvuta Rodrygo akiwa anakwenda kufunga, mabao ya Real Madrid yamefungwa na Karim Benzema dakika ya 21 na Marco Asensio dakika ya 74.
  Timu hizo zitarudiana Aprili 18 Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London na mshindi wa jumla atakwenda Nusu Fainali.
  Robo Fainali nyingine ya kwamza ya Ligi ya Mabingwa usiku wa Jumatano, bao pekee la Ismael Bennacer dakika ya 40 liliipa AC Milan ushindi wa 1-0 dhidi ya Napoli Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan.
  Timu hizo zitarudiana Aprili 18 Uwanja wa Diego Armando Maradona Jijini Napoli na mshindi wa jumla atakwenda Nusu Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YAICHAPA CHELSEA 2-0, AC MILAN 1-0 NAPOLI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top