• HABARI MPYA

  Wednesday, April 12, 2023

  SUGU AAHIDI SH MILIONI 1 KILA BAO LA USHINDI MBEYA CITY


  ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Mbeya, Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’ ameahidi kutoa Sh. Milioni kwa mchezaji atakayefunga kila bao la ushindi kuanzia sasa Mbeya City katika kampeni ya kuinusuru timu isishuke Daraja.
  “Mbeya Simameni!! Timu yetu iko hatarini kushuka daraja, Tusikubali!
  Tumebakiza mechi nne na ili kupona inabidi tushinde hata mechi mbili tu,”amesema Mbilinyi maarufu kama Sugu na kuongeza;
  “Katika kuhamasisha wachezaji wetu uwanjani, mimi nitatoa Sh. Milioni 1 kwa kila goli la ushindi kwenye mechi zote zilizobaki na mkwanja utaenda kwa Mfungaji,” amesema Mbilinyi ambaye umaarufu wake ulianzia kwneye muziki wa Bongo Fleva miaka ya 1990.
  Kwa sasa Mbeya City inashika nafasi ya 13 kwa pointi zake 27, ikifuatiwa na KMC pointi 26, Ruvu Shooting 20 na Polisi Tanzania 19 baada ya wote kucheza mechi 26.
  Ikumbukwe mwishoni mwa msimu timu mbili zitashuka moja kwa moja, wakati watakaomaliza nafasi ya 13 na 14 watamenyana baina yao timu itakayofungwa baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini itakwenda kucheza timu ya Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SUGU AAHIDI SH MILIONI 1 KILA BAO LA USHINDI MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top