
WENYEJI, Namungo FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Jacob Massawe dakika ya 23 na Shiza Kichuya dakika ya 74, wakati la Mbeya City limefungwa na Abdulrazak Mohamed dakika ya 88.
Kwa ushindi huo wanafikisha pointi 35 na kupanda nafasi ya tano, huku Mbeya City ikibaki na pointi zake 27 nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi 26.
0 comments:
Post a Comment