• HABARI MPYA

  Wednesday, April 12, 2023

  KWA HAT -TRICK BOCCO NDIYE 'BABA LAO' LIG KUU


  NAHODHA wa Simba SC, John Raphael Bocco ndiye mchezaji aliyefunga mabao matatu kwenye mechi moja zaidi ya mara moja msimu huu wa Ligi Kuu ya Tanmzania Bara.
  Bocco, mchezaji wa zamani wa Cosmopolitan na Azam FC zote za Dar es Salaam japo ana mabao tisa tu msimu huu kwenye Ligi Kuu, lakini ana hat-trick mbili.
  Wanaomfuatia ni wachezaji wenzake wa Simba, Mkongo Jean Baleke na Mrundi, Saido Ntibanzokiza ambao kila mmoja ana hat-trick moja sawa na Fiston Mayele, Stephanie Azizi Ki wote wa Yanga na Ibrahim Mkoko wa Namungo FC.
    

     


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KWA HAT -TRICK BOCCO NDIYE 'BABA LAO' LIG KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top