• HABARI MPYA

  Monday, April 10, 2023

  KOCHA NABI AREJEA YANGA BAADA YA KUKOSEKANA WIKI MBILI


  KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Mtunisia Nasredine Nabi amerejea nchini baada ya mapumziko ya wiki mbili na leo ameanza kuinoa timu kuelekea mechi na Kagera Sugar keshokutwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Nabi hakuwepo Yanga ikipata ushindi mwembamba wa 1-0 mara mbili katika mechi mbili zilizopita ugenini na nyumbani katika michuano tofauti.
  Kwanza ni ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, TP Mazembe kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika Jijini Lubumbashi Aprili 2 na baadaye Jumamosi dhidi ya Geita Gold katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu Azam Sports Federation Cup (ASFC). 
  Baada ya mchezo wa Jumanne na Kagera Sugar Yanga itarejea kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya watani, Simba SC Aprili 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA NABI AREJEA YANGA BAADA YA KUKOSEKANA WIKI MBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top