• HABARI MPYA

  Thursday, April 13, 2023

  JULIO KOCHA MPYA KMC, HITIMANA ATIMULIWA  UONGOZI wa KMC umemfuta kazi Kocha Mnyarwanda, Thierry Hitimana na wasaidizi wake wote nafasi yake kuchukuliwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye anaingia na wasaidizi wake.
  Hitimana anaondolewa kutokana na mwenendo mbaya wa timu, hadi sasa ikiwa inashika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 26, ikifuatiwa na Ruvu Shooting pointi 20 na Polisi Tanzania pointi 19.
  Ikumbukwe mwishoni mwa msimu timu mbili zitakazoshika nafasi za mwisho, 15 na 16 zitashuka moja kwa moja.
  Aidha, timu zitakaomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao na itakayofungwa baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini itakwenda kucheza timu ya Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JULIO KOCHA MPYA KMC, HITIMANA ATIMULIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top