• HABARI MPYA

  Wednesday, April 12, 2023

  DIARRA AFIKISHA CLEEN SHEETS 15 ZA MSIMU WA LIGI KUU

  KIPA wa Kimataifa wa Mali, Djigui Diarra wa Yanga jana alifikisha mechi 15 za kusimama langoni bila kuruhusu bao, timu yake ikiibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Diarra aliye katika msimu wake wa pili Yanga sasa anendelea kuongoza miongoni mwa makipa wa Ligi Kuu kwa kudaka mechi nyingi bila kufungwa, akifuatiwa na Aishi Salum Manula wa Simba SC mwenye mechi 12 za kutoruhusu bao na Mcomoro wa Azam FC, Ali Ahamada mwenye mech nane.

   


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DIARRA AFIKISHA CLEEN SHEETS 15 ZA MSIMU WA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top