• HABARI MPYA

  Monday, May 02, 2022

  MTIBWA SUGAR YATOA SARE 1-1 NA BIASHARA NYAMAGANA


  TIMU ya Mtibwa Sugar imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, wahamiaji Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
  Aliyeisaidia Mtibwa kupata pointi moja ugenini leo ni mshambuliaji Mrundi, Nzigamasabo Steve aliyefunga bao la kusawazisha dakika ya 90 na ushei, kufuatia Nassib Mpapi kuanza kuifungia Biashara dakika ya 44.
  Mtibwa Sugar inafikisha pointi 24 baada ya sare hiyo na kusogea nafasi ya 10, wakati Biashara pamoja na kufikisha pointi 23 inabaki nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YATOA SARE 1-1 NA BIASHARA NYAMAGANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top