• HABARI MPYA

  Sunday, May 01, 2022

  ANCELOTTI AIPA REAL MADRID TAJI LA LA LIGA


  KOCHA mkongwe Mtaliano, Carlo Ancelotti ameweka rekodi ya kushinda mataji ya ligi zote kubwa Ulaya baada ya jana kuiwezesha Real Madrid kutwaa ubingwa wa La Liga nchini Hispania.
  Real Madrid imejihakikishia taji la La Liga msimu huu baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Espanyol jana Uwanja Santiago Bernabéu Jijini Madrid, mabao ya Rodrygo dakika ya 33 na 43, Asensio dakika ya 55 na Karim Benzema dakika ya 81, hivyo kufikisha pointi 81 katika mchezo wa 34, ambazo haziwezi kufikiwa na wapinzani.
  Ancellotti anabeba taji la La Liga baada ya awali kushinda mataji ya Ligi za nyumbani kwao, Italia, England, Ufaransa na Ujerumani hivyo kuwa kocha wa kwanza kubeba mataji ya ligi tano kubwa Ulaya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ANCELOTTI AIPA REAL MADRID TAJI LA LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top