• HABARI MPYA

  Saturday, January 02, 2021

  TAIFA STARS WAANZA MAZOEZI KUJIANDAA NA MECHI MBILI ZA KIRAFIKI DHIDI YA DRC KUJIANDAA NA CHAN 2021

  BEKI mpya wa timu ya soka taifa ya Tanzania, Taifa Stars akiwa mazoezini leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kujiandaa na michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Januari 10 na 13.

  Kiungo Feisal Salum akijiandaa na mechi hizo ni mechi maalum za Taifa Stars kujiandaa na Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN),  zitakazofanyika nchini Cameroon kuanzia Januari 16 hadi Februari 7, mwaka huu.

  Kiungo Farid Mussa akijiandaa na CHAN, michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, Tanzania imepangwa Kundi D pamoja na Zambia, Guinea na Namibia.

  Kundi linaundwa na Cameroon, Mali, Burkina Faso na Zimbabwe, Kundi B; Libya, DRC, Kongo na Niger na Kundi C lina mabingwa watetezi Morocco, Rwanda, Uganda na Togo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS WAANZA MAZOEZI KUJIANDAA NA MECHI MBILI ZA KIRAFIKI DHIDI YA DRC KUJIANDAA NA CHAN 2021 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top