• HABARI MPYA

  Alhamisi, Septemba 05, 2019

  KCB WASAINI MKATABA MPYA WA MWAKA MMOJA KUENDELEA KUWA WADHAMINI WA LIGI KUU

  Na Saada Salim, DAR ES SALAAM
  BENKI ya KCB imesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. 
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano baada ya kusaini mkataba huo wenye thamani ya shilingi Milioni 495 pamoja na Kodi, KCB wataendelea kuwa wadhamini wa Ligi Kuu kwa msimu mwingine.
  KCB wanaungana na Kampuni ya Vodacom Tanzania ambao mwezi uliopita walisaini mkataba wa miaka mitatu kurejesha udhamini katika Ligi baada ya mwaka mmoja uliopita kujiweka kando kufuatia kutofautiana na TFF.

  Vodacom haikusaini mkataba mpya wa kuendelea kudhamini Ligi Kuu msimu uliopita kufuatia kutofikia makubaliano na TFF, huku sababu kubwa ikielezwa ni ongezeko la timu kutoka 16 hadi 20.
  Lakini baada ya makubaliano ya kupunguza idadi ya timu kuanzia msimu huu, leo Vodacom na TFF wameingia mkataba huo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 9, yaano Sh Bilioni 3 kwa mwaka, ikiwa ni ongezeko la Sh Bilioni 2.4 kutoka mkataba uliomalizika mwaka 2018.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KCB WASAINI MKATABA MPYA WA MWAKA MMOJA KUENDELEA KUWA WADHAMINI WA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top