• HABARI MPYA

    Saturday, November 04, 2017

    MSUVA TAYARI YUPO DAR ES SALAAM KUJIUNGA NA TAIFA STARS

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    WINGA wa Difaa Hassan El Jadida ya Moroccco, Simon Happygod Msuva amewasili leo mjini Dar es Salaam kujiunga na kikosi cha timu ya taifa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Benin wiki ijayo. 
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Msuva amesema kwamba amewasili leo asubuhi mjini Dar es Salaam kutoka Morocco tayari kujiunga na Taifa Stars.
    Wachezaji wengine wa Taifa Stars wanaocheza nje, akiwemo Nahodha Mbwana Ally Samatta anayecheza KRC Genk ya Ubelgiji wanatarajiwa kuwasili kuanzia leo.
    Simon Msuva (kushoto) amefunga mabao yote matatu ya Taifa Stars katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Botswana na Malawi 

    Msuva amefunga mabao yote matatu ya Taifa Stars katika mechi mbili zilizopita, ikishinda 2-0 dhidi ya Botswana Septemba 3 na ikitoa sare ya 1-1 na Malawi Oktoba 7, Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. 
    Na baada ya kucheza nyumbani mfululizo mechi za kirafiki za kimataifa, Taifa Stars sasa itatoka mwezi huu kwenda Benin kucheza na wenyeji Novemba 11, mwaka huu na kikosi cha wachezaji 24 kitaingia kambini kesho mjini Dar es Salaam kabla ya kusafiri Novemba 9 kwenda Benin tayari kwa mchezo huo.  
    Kikosi kamili cha Taifa Stars sasa ni makipa; Aishi Manula (Simba SC), Peter Manyika (Singida United) na Ramadhani Kabwili, mabeki Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Gardiel Michael (Yanga), Kevin Yondan (Yanga), Nurdin Chona (Prisons) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).
    Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Mudathir Yahya (Singida United), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Jonas Mkude (Simba), Raphael Daudi (Yanga), Simon Msuva (Yanga), Shiza Kichuya (Simba), Ibrahim Hajib (Yanga), Mohammed Issa (Mtibwa), Farid Mussa (Tenerife/Hispania) na Abdul Mohammed (Tusker/Kenya) na washambuliaji Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Mbaraka Yussuf (Azam FC), Elias Maguri (Huru) na Yohanna Nkomola (Huru).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSUVA TAYARI YUPO DAR ES SALAAM KUJIUNGA NA TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top