• HABARI MPYA

  Sunday, October 01, 2017

  SAMATTA MAMBO MAGUMU GENK, WAMETOA SARE NYINGINE TENA UBELGIJI


  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amecheza dakika zote 90 timu yake, KRC Genk ikilazimisha sare ya 3-3 na wenyeji, KAS Eupen katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A, Ubelgiji usiku wa Jumamosi Uwanja wa am Kehrweg mjini Eupen. 
  Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Nathan Verboomen, wenyeji walitangulia kwa mabao mawili kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Siebe Blondelle dakika ya 12 na Akram Afif dakika ya 40, wote wakisetiwa na Luis Garcia.
  Genk wakazinduka kipindi cha pili na kupata bao la kwanza lililofungwa na Marcus Ingvartsen dakika ya 53, akimalizia pasi ya Clinton Mata, kabla ya wenyeji kufunga la tatu kupitia kwa M'Baye Leye dakika ya 57, kwa pasi ya Akram Afif.
  Genk wakapambana tena hadi kusawazisha mabao hayo kupitia kwa Siebe Schrijvers dakika ya 66 na Marcus Ingvartsen dakika ya 78. 
  Samatta amefikisha mechi 65 za mashindano yote tangu Januari mwaka jana alipojiunga na Genk, akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Katika mechi hizo, Samatta ambaye ni mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika mwaka jana alipokuwa na Mazembe, 37 alianza na mechi 24 alitokea benchi.
  Katika mechi hizo, mshambuliaji huyo wa zamani wa African Lyon, zamani Mbagala Market na Simba zote za Dar es Salaam, amefunga jumla ya mabao 21 kwenye mashindano yote.
  Baada ya mchezo huo, Mbwana anatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu kujiunga na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi Oktoba 7, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 
  Kikosi cha KAS Eupen kilikuwa: Van Crombrugge, Amani/George dk90, Leye, Garcia, Afif /Sanhaji dk91, Wague, Blondelle, Tirpan, Ocansey, Valiente and Verdier/Schouterden).
  KRC Genk : Vukovic, Colley, Brabec/Khammas dk45, Aidoo, Writers/Benson dk76, Malinovskyi, Berge, Mata/Maehle dk76, Pozuelo, Ingvartsen na Samatta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA MAMBO MAGUMU GENK, WAMETOA SARE NYINGINE TENA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top