• HABARI MPYA

  Monday, September 04, 2017

  RATIBA MPYA YA LIGI KUU YATOKA, SIMBA KUIFUATA AZAM CHAMAZI JUMAMOSI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RATIBA iliyofanyiwa marekebisho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imetoka leo na mchezo kati ya Azam FC na Simba SC utafanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Septemba 9, mwaka huu.
  TFF imeamua kuanzia sasa Azam FC wautumie Uwanja wao wa nyumbani, Azam Complex kwa mechi zao zote za nyumbani kuanzia na huo wa Simba – tofauti na miaka ya nyuma walipotakiwa kuwafuata vigogo Simba na Yanga Uwanja wa Taifa na Uhuru.   
  Na Simba SC wameyapokea kwa moyo mkunjufu mabadiliko hayo – kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, Hajji Sunday Manara wamesema wanakwenda Azam Complex kwa moyo mkunjufu.
  Kiungo mpya wa Simba, Haruna Niyonzima atakuwa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam
  “Tunakwenda Chamazi tukijiamini na tunaamini huu ni mwanzo mzuri, Azam hawana budi kutushukuru pasi na ukakasi kuonyesha utayari na dhamira yetu njema ya kutaka wapate fursa ya kuutumia Uwanja wao,”amesema Manara. 
  Kiongozi huyo wa Simba ameipongeza TFF kwa kuwaruhusu Azam kutumia uwanja wao wa Chamazi kwenye mechi za Simba na Yanga hata kama ni mdogo.
  “Mawazo yangu yananiambia wamefanya uwekezaji mkubwa na wanapaswa kuonyeshwa shukrani kwa mechi zao zote za nyumbani kuchezewa pale. Naamini wana miundombinu ya kutosha na hii itakuwa fundisho kwetu kwa Yanga na Simba kujenga vya kwetu,”ameongeza. GONGA HAPA KUTAZAMA RATIBA MPYA KAMILI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RATIBA MPYA YA LIGI KUU YATOKA, SIMBA KUIFUATA AZAM CHAMAZI JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top