• HABARI MPYA

  Friday, September 01, 2017

  OKWI AIPAISHA UGANDA KUNDI E KUFUZU KOMBE LA DUNIA

  MSHAMBULIAJi wa Simba, Emmanuel Arnold Okwi jana aliibuka shujaa wa timu yake ya taifa, Uganda baada ya kufunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Misri.
  Okwi, aliyerejea Simba mwezi uliopita, alifunga bao hilo katika mchezo wa Kundi E kufuzu Fainali za Kombe la Dunia Urusi mwaka 2018 uliofanyika Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala.
  Aliwapiga chenga mabeki wa Mafarao baada ya kupokea pasi ya mchezaji mwenzake wa Simba, beki Juuko Murshid na kufumua shuti kali lililomshinda kipa mkongwe, Essam El Hadary.
  Kwa ushindi huo, Uganda sasa inaongoza Kundi E baada ya kufikisha pointi saba kufuatia kucheza mechi tatu, ikifuatiwa na Misri yenye pointi sita, Ghana pointi moja wakati Kongo hawana kitu.
  Kikosi cha Uganda kilikuwa; Denis Onyango, Geoffrey Walusimbi, Isaac Isinde, Joseph Ochaya/Isaac Muleme dk90+7, Nico Wadada, Juuko Murshid, Hassan Wasswa, Khalid Aucho, Faruk Miya/Kizito Luwagga dk75, Emmanuel Okwi/Geofrey Sserunkuma dk88 na Derrick Nsimbambi.
  Misri; Essam El Hadary, Ahmed Fathy, Mohamed Abdul Shafy, Ahmed Hegazi, Rami Rabia, Abdalla El Said, Mohamed Elneny, Kahraba/Amr Gamal dk67, Trezeguet/Ramadan Sobhi d46, Tarek Hamed/Saleh Gomaa dk73 na Mohamed Salah.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OKWI AIPAISHA UGANDA KUNDI E KUFUZU KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top