• HABARI MPYA

  Friday, September 01, 2017

  AZAM FC WAJIPIMA NA TRANS CAMP LEO CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC leo inateremka kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kukipiga na Trans Camp, katika mchezo wa kirafiki kuanzia saa 10.00 jioni.
  Mchezo huo ni maalum kabisa kwa ajili ya benchi la ufundi la Azam FC chini ya Kocha Mkuu Aristica Cioaba, kuwaweka katika ushindani wachezaji wake kutokana na wikiendi hii kutokuwa na mchezo wowote wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
  Aidha atautumia pia kama sehemu ya kukisoma kikosi chake kabla ya kuvaana na Simba Jumatano ijayo katika mchezo wa ligi, utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex.
  Kikosi cha Azam FC kipo kwenye hali nzuri na morali ya hali ya juu kuelekea mtanange huo muhimu, ambapo wachezaji wanaari kubwa ya kuzoa pointi zote tatu kwa ajili ya kujenga heshima na kujiweka sawa kwenye mbio za ubingwa wa ligi.
  Mshambuliaji tegemeo wa Azam FC, Yahya Mohammed (kulia) anataraiwa kuendeleza makali yake leo
  Katika mchezo wa kwanza wa ligi, Azam FC inayodhaminiwa na maji safi ya Uhai Drinking Water, Benki bora ya NMB na Tradegents, ilishinda ugenini mkoani Mtwara kwa kuichapa Ndanda ya huko bao 1-0, lililofungwa kwa kichwa na mshambuliaji Yahaya Mohammed, akimalizia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Bruce Kangwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC WAJIPIMA NA TRANS CAMP LEO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top