• HABARI MPYA

    Monday, July 06, 2015

    NI PATIKASHIKA LEO CHOLE UNITED VS CHOLE RANGERS KOMBE LA MWEZI MTUKUFU DIAMOND

    Chole United leo watakutana na ndugu zao Rangers (chini) katika Nusu Fainali Kombe la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
    TIMU za Chole Rangers na Chole United zimefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Mwezi mtukufu wa Ramadhani na leo zitamenyana zenyewe.
    Katika michuano hiyo inayoendelea kwenye Uwanja wa shule ya Msingi Diamond, Upanga mjini Dar es Salaam, Chole United iliifunga Young Legends mabao 4-0, wakati Rangers iliifunga DFC Mekone 1-0.
    Mabao ya United yalifungwa na Lutfy Bin Kleb ambaye pia ni wakala wa wachezaji anayetambuliwa na FIFA na Osama Muchacho kila mmoja mawili, wakati bao pekee la ushindi la Rangers lilifungwa na Salim Moro Best.
    Lutfy ambaye ni mdogo wa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Abdallah Bin Kleb ndiye anaongoza kwa mabao katika michuano hiyo inayofanyika usiku, akiwa amefunga manne sawa na Mohammed Saadat wa Saggar FC, wakifuatiwa na Osama Muchacho wa Chole United pia na Seedon wa DFC United wenye mabao matatu kila mmoja.    
    Nusu Fainali zitachezwa leo usiku, Chole United na Rangers zikimenyana zenyewe wakati Nusu Fainali nyingine itakuwa kati ya DFC United na Saggar.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI PATIKASHIKA LEO CHOLE UNITED VS CHOLE RANGERS KOMBE LA MWEZI MTUKUFU DIAMOND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top