MAREKANI ndiyo mabingwa wa Kombe la Dunia wanawake 2015- baada ya kuwafunga waliokuwa mabingwa watetezi, Japan kwa mabao 5-2 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa BC Place mjini Vancouver, Canada.
Carli Lloyd alifunga mabao mawili dakika tano za mwanzo (ya tatu na ya tano) kabla ya Lauren Holiday kufunga la tatu dakika ya 14.
Kiungo Lloyd akakamilisha hat-trick yake dakika ya 16, kabla ya Yuki Ogimi kuifungia Japan la kwanza dakika ya 27 na Julie Johnston wa Marekani akajifunga dakika ya 52 kuwapatia wapinzani bao la pili.
Katika fainali hiyo ambayo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi alihudhuria, Tobin Heath alinogesha sherehe za Marekani kwa bao safi la tano dakika ya 54.
Kikosi cha Marekani kilikuwa; Solo, Krieger, Johnston, Sauerbrunn, Klingenberg, Heath/Wambach dk79, Holiday, Brian, Rapinoe/O'Hara dk61, Morgan/Rampone dk86 na Lloyd.
Japan: Kaihori, Ariyoshi, Iwashimizu/Sawa dk33, Kumagai, Sameshima, Kawasumi/Sugasawa dk39, Sakaguchi, Utsugi, Miyama, Ohno/Iwabuchi dk60 na Ogimi.
Kipa Hope Solo (katikati) akiinua Kombe la Dunia wakati wakisherehekea na wachezaji wenzake baada ya ushindi dhidi ya Japan PICHA ZAIDI GONGA HAPA



.png)
0 comments:
Post a Comment