• HABARI MPYA

    Tuesday, July 07, 2015

    KIPRE TCHETCHE AING’ARISHA AZAM FC DHIDI YA JKT RUVU CHAMAZI

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche ametokea benchi kuifungia Azam FC bao pekee la ushindi ikiilaza JKT Ruvu 1-0 katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Kipre aliyeingia kuchukua nafasi ya Didier Kavumbangu dakika ya 80 aliifungia Azam FC bao hilo baada ya dakika tano tu akiunganisha krosi ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
    JKT Ruvu iliyoongozwa na mshambuliaji wa zamani wa Mbeya City na Rhino Rangers, Saad Kipanga ilionyesha upinzani kwa Azam FC na haikuwa bahati yao tu kupata bao.
    Kipindi cha kwanza timu hizo zilishambuliana kwa zamu na ni JKT Ruvu ndio waliofika mara nyingi langoni mwa Azam FC, lakini kipa Aishi Salum Manula alikuwa vizuri leo kuokoa hatari zote.
    Kipre Tchetche (kulia) akiwatoka mabeki wa JKT Ruvu leo Chamazi
    Kevin Friday (kulia) akipambana na beki w JKT Ruvu leo Chamazi

    Kavumbangu na Kelvin Friday walioanza pamoja mbele leo Azam FC, walikosa maarifa ya kumtungua kipa Tony Kavishe wa JKT Ruvu.
    Kocha wa JKT Ruvu, Freddy Felix Minziro aliwaanzisha vijana wengi aliowapandisha kutoka timu ya vijana na wakacheza soka nzuri iliyowasisimua wengi.
    Kocha Muingereza wa Azam FC, alimuacha benchi kipa wake mpya kutoka Ivory Coast, Vincent Atchouailou de Paul Angban aliyewahi kudakia timu ya vijana ya klabu bingwa England, Chelsea FC.
    Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Kipre Balou/Bryson Raphael, David Mwantika/Said Mourad, Aggrey Morris, Abdallah Kheri/Serge Wawa, Himid Mao, Erasto Nyoni, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Kevin Friday/Malik Mussa/Brian Majwega/Gardiel Michael na Didier Kavumbangu/Kipre Tchetche.
    JKT Ruvu; Tony Kavishe, Napho Zubeiry, Jaffar Kisoky, Kisimba Luambano, Martin Kazila/Bhinda Abdallah, Hamisi Shengo, Ismail Aziz, Mateo Saad/Yohana Misanya, Alex Abel, Saad Kipanga na Emmanuel Pius/Daud John.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIPRE TCHETCHE AING’ARISHA AZAM FC DHIDI YA JKT RUVU CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top