• HABARI MPYA

    Sunday, June 14, 2015

    ROONEY APIGA LA USHINDI ENGLAND YAUA 3-2 MBIO ZA EURO 2016

    ENGLAND imepata ushindi wa mabao 3-2 ugenini dhidi ya Sloveania mchezo wa Kundi E kufuzu Euro 2016 usiku huu.
    Milivoje Novakovic alianza kuifungia Slovenia dakika ya 37 kabla ya Jack Wilshere kuisawazishia England dakika ya 57, hilo likiwa bao lake la kwanza kuifungia Three Lions.
    Wilshere akaifungia tena England bao la pili dakika ya 73, kabla ya Nejc Pecnik kuisawazishia Slovenia dakika ya 84.
    Shujaa wa mchezo wa leo alikuwa Wayne Rooney aliyeifungia England bao la ushindi dakika ya 86.
    Kikosi cha Slovenia kilikuwa; Handanovic, Brecko, Ilic, Cesar, Jokic, Mertelj, Kurtic, Illcic/Birsa dk61, Kampl, Kirm/Pecnick dk72 na Novakovic.
    England; Hart, Jones/Lallana dk46, Cahill, Smalling, Gibbs, Henderson, Wilshere, Delph/Clyne dk86, Townsend/Walcott dk74, Rooney na Sterling.
    Wayne Rooney's 86th minute goal, his 48th for England, handed victory to Roy Hodgson's side in Slovenia in a tough match
    Wayne Rooney akishangilia baada ya kuifungia England bao la ushindi dakika ya 86 dhidi ya Slovenia usiku huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ROONEY APIGA LA USHINDI ENGLAND YAUA 3-2 MBIO ZA EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top