Na Mwandishi Wetu, BUKOBA
BAO pekee la kiungo Paul Ngway, dakika ya 52 jioni ya leo limeipa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga SC, Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga SC ilimaliza mchezo huo pungufu, baada ya Nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 80 na refa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, baada ya kumpiga kichwa Rashid Mandawa wa Kagera.
Ngway, mchezaji mkongwe wa timu hiyo ya Wakata Miwa wa Misenyi, Bukoba Vijijini, alifunga bao zuri kwa shuti kali akimalizia krosi ya Julius Kwangwa.
Yanga SC inabaki na pointi zake 10 baada ya mechi sita, ikishinda tatu, sare moja na kufungwa mbili, nyingine na Mtibwa Sugar mjini Morogoro 2-0.
Baada ya mchezo huo, mashabiki wa Yanga SC walimtisha refa kiasi cha kutolewa uwanjani kwa msaada wa askari wa Polisi.
Kagera Sugar; Agathon Anthony, Benjamin Asukile, Abubakar Mtiro, Erick Kyaruzi, George Kavilla, Babu Ally, Julius Ambrose, Paul Maona, Rashid Mandawa, Atupele Green na Adam Kingwande/Paul Ngway dk46.
Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/Nizar Khalfan dk87, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima/Hamisi Kiiza dk72, Genilson Santos ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho/Jerry Tegete dk54.

0 comments:
Post a Comment