![]() |
| Solomon Kalou alifunga mawili |
Mchezo huo ulioshuhudiwa na umati mkubwa wa watu Abidjan, ulifurahia mabao yaliyofungwa na nyota wao, Salomon Kalou mawili, Kolo Toure, Max Gradel na Gervinho.
Bao la kufutuia machozi la Sierra Leone lilifungwa na Mustapha Bangoura aliyegongeana vizuri na Alhassan Kamara.
Ushindi huo unawafanya Tembo hao wafikishe pointi tisa, moja nyuma ya vinara wa kundi lao, Cameroon ambao leo wanacheza na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), yenye pointi sita.
Kikosi cha Sierra Leone kilikuwa: Solomon Zombo Morris, Alie Sesay, David Simbo, Mustapha Dumbuya, John Kamara, Lansana Kamara, Mohamed Kamara, Mustapha Bangura, Hassan Sesay, Sherif Suma na Alhassan Kamara
Ivory Coast: Sylvain Gbohouo, Kolo Toure, Siaka Tiene, Ousmane Viera Diarassouba, Serge Aurier, Yaya Toure, Geoffroy Serey Die, Max Gradel, Salomon Kalou, Gervinho na Lacina Traore.



.png)
0 comments:
Post a Comment