• HABARI MPYA

    Saturday, November 15, 2014

    RONALDO AFUNGA BAO URENO IKICHINJA 1-0 NA KUWEKA REKODI NYINGINE YA HESHIMA ULAYA

    URENO imeilaza bao 1-0 Armenia mjini Faro usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Kundi I kufuzu Kombe la Mataifa ya Ulaya, maarufu kama Euro 2016.
    Shukrani zimuendee Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 71 kuipatia pointi muhimu nchi yake katika mbio hizo- ambalo linakuwa bao lake la 23 kwenye mechi za kufuzu za Euro na kuweka rekodi ya mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye michuano hiyo. 
    Ushindi huo, unaifanya Ureno ifikishe pointi sita baada ya kucheza mechi tatu na kupanda nafasi ya pili kwenye kundi hilo, nyuma ya Denmark wanaoongoza kwa pointi zao saba za mechi nne.
    Albania ina pointi nne za mechi tatu, wakati Serbia na Armenia zina pointi moja kila moja baada ya kucheza mechi tatu.   
    Aidha, kwa mshambuliaji huyo wa klabu bingwa Ulaya, Real Madrid- Ronaldo kutokana na kufunga bao hilo pekee jana, anakuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye michuano hiyo ya Ulaya.
    Kikosi cha Ureno kilikuwa; Patricio, Bosingwa, Pepe, Carvalho, Guerreiro, Nani/Carvalho, Moutinho, Tiago, Ronaldo, Postiga/Eder na Danny/Quaresma.
    Armenia: Berezovsky, Hovhannisyan, Haroyan, Arzumanyan, Taron Voskanyan, Hayrapetyan, Mkrtchyan/Pizzelli, Mkhitaryan, Yedigaryan/Sarkisov, Ghazaryan/Manucharyan na Movsisyan. 
    The Real Madrid superstar wheels away after breaking yet another record in his illustrious career for club and country
    Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kufunga jana
    Ronaldo, wearing his new black CR7 branded boots, dribbles the ball past Varazdat Haroyan of Armenia
    Ronaldo, alivalia viatu vyake vipya vyeusi vya CR7 na hapa anamtoka Varazdat Haroyan wa Armenia

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2835268/Portugal-1-0-Armenia-Cristiano-Ronaldo-pokes-home-highest-goal-scorer-European-Championship-history.html#ixzz3J688uBFe 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO AFUNGA BAO URENO IKICHINJA 1-0 NA KUWEKA REKODI NYINGINE YA HESHIMA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top