'Bwana mikogo', bingwa wa madaraja matano tofauti ya uzito katika ndondi, Floyd Mayweather ameposti video kwenye intaneti akiwa amezungukwa na 'mahela' kama kawaida yake.
Katika kipande hicho kifupi cha video alichoposti kwenye akaunti yake ya Instagram, anaonyesha dola za Kimarekani bilioni 100 katikati ya chumba chake.
Mbabe huyo ambaye hajawahi kupoteza pambano wakati 'mahela' hayo yakiwa mbele yake, yeye hana habari anacheza na simu yake tu huku amevalia kofia iliyoandikwa '$1m', yaani dola milioni moja.
Floyd Mayweather ameposti video akionyesha 'mahela' kama kawaida yake
0 comments:
Post a Comment