KIPA David De Gea anaweza kuwa nje ya Uwanja hata kwa mwezi mzima baada ya kuumia kidole wakati wa mazoezi ya timu yake ya taifa, Hispania.
Mlinda mango huyo wa Manchester United alifanyiwa uchunguzi na timu ya matabibu wa Hispania Ijumaa usiku kabla ya kuamua line atarejea Old Trafford.
Kipa mwenye umri wa miaka 24 ambaye amekuwa kwenye kiwango kizuri United msimu huu, aliumia kidole kidogo cha mkono wa kulia wakati anajaribu kuokoa shut la Paco Alcacer mazoezini wakijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Belarus mjini Huelva.
David de Gea akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuumia kwenye mazoezi ya Hispania jana
De Gea akiondoka uwanjani mjini Huelva jana baada ya kuumia
Mara moja mchezaji huyo alitoka nje baada ya kupatiwa huduma ya kwanza na kugundulika maumivu yake ni makubwa kidogo, na United imethibitisha kupewa taarifa na Chama cha Soka Hispania juu hya kuumia kwa kipa wao huyo.
Hilo ni pigo lingine kwa Hispania, kwani tayari watamkosa kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas anayesumbuliwa na maumivu ya nyama.


.png)
0 comments:
Post a Comment