• HABARI MPYA

    Monday, November 17, 2014

    PIGO MAN UNITED, BLIND AUMIA GOTI AKIICHEZEA UHOLANZI KUFUZU EURO JANA

    KIUNGO Daley Blind anaweza kuwa nje ya Uwanja kwa wiki kadhaa baada ya kuumia mguu jana akiichezea Uholanzi ikishinda 6-0 dhidi ya Latvia.
    Hilo ni pigo kwa klabu yake, Manchester United, baada ya Blind kuanguka chini dakika ya 19 Uwanja wa Amsterdam Arena, kufuatia kugongwa gotini na Eduards Visnakovs. Hiyo ni mara ya 39 Blind anaumia United tangu kocha Louis van Gaal aanze kazi Julaim, ambayo ni wastani wa kuumia mara moja katika kila siku tatu.
    Pamoja na kuumia kwa Blind, lakini kocha wa Uholanzi, Guus Hiddink hajaonyesha wasiwasi sana juu ya maumivu ya mchezaji huyo, akiamini si muda mrefu. 
    The Manchester United midfielder looks in real pain while clutching his left knee during Holland's game with Latvia on Sunday
    Kiungo wa Manchester United akiugulia maumivu jana baada ya kuumizwa goti

    MECHI AMBAZO BLIND ANAWEZA KUZIKOSA 

    Novemba 22: dhidi ya Arsenal ugenini 
    Novemba 29: dhidi ya Hull City nyumbani  
    Desemba 2: dhidi ya Stoke City nyumbani
    Deesemba 8: dhidi ya Southampton ugenini
    Deesemba 14: dhidi ya Liverpool nyumbani
    Desemba 20: dhidi ya Aston Villa ugenini
    Desemba 26: dhidi ya Newcastle United nyumbani 
    Desemba 28: dhidi ya Tottenham Hotspur ugenini
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO MAN UNITED, BLIND AUMIA GOTI AKIICHEZEA UHOLANZI KUFUZU EURO JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top