• HABARI MPYA

    Sunday, November 16, 2014

    MWADUI, TOTO NA RANGERS ZOTE ZATOA SARE MBIO ZA LIGI KUU LEO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    FRIENDS Rangers imepunguzwa kasi na Kimondo baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza jioni ya leo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
    Rangers ya kocha Ally Yussuf ‘Tigana’ ilitangulia kupata bao kupitia kwa Samuel Mathayo dakika ya 11, kabla ya Sunday William kuisawazishia Kimondo dakika ya 23.
    Almasi Mkinda aliinyima Rangers nafasi ya kuondoka na pointi tatu baada ya kukosa penalti na timu hiyo Manzese inabaki nafasi ya pili Kundi A kwa kufikisha pointi 20, nyuma ya Majimaji wenye pointi 21, baada ya timu zote kucheza mechi 10.
    Rangers wamepunguzwa kasi leo Daraja la Kwanza

    Katika mechi nyingine za leo, Rhino imetoka sare ya 1-1 na Toto Uwanja wa Mwinyi, Tabora, African Lyon imeshinda 1-0 dhidi ya KMC, Polisi Mara imetoka sare ya 2-2 na Geita Gold Mine na Burkina Faso imetoka sare ya 1-1 na Mwadui FC.
    Matokeo haya yanaifanya Toto izidi kujitanua kileleni mwa Kundi B baada ya kufikisha pointi 23 za mechi 11, ikifuatiwa na Mwadui yenye pointi 16 za mechi tisa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWADUI, TOTO NA RANGERS ZOTE ZATOA SARE MBIO ZA LIGI KUU LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top