• HABARI MPYA

    Tuesday, November 18, 2014

    MAN UNITED YAKABILIWA NA TATIZO LA KIPA KUELEKEA MECHI NA ARSENAL JUMAMOSI EMIRATES

    KLABU ya Manchester United haijafanya utaratibu wowote wa kumsajili kipa Victor Valdes kwa ajili ya Ligi Kuu ya England wiki hii, hivyo hataweza kucheza dhidi ya Arsenal Jumamosi wiki hii.
    United inakabiliwa na tatizo la majeruhi na viungo Daley Blind na Michael Carrick na kipa David de Gea nao wamerejea kutoka kwenye majukumu ya kimataifa wakiwa majeruhi.
    De Gea aliyeumia kidole yuko shakani kudaka mwishoni mwa wiki – na bado haijathibitishwa rasmi ingawa kuna tetesi kocha wa United, Louis van Gaal anaweza kumgeukia kipa namba mbili, Anders Lindegaard Uwanja wa Emirates wikiendi hii.
    Man United goalkeeper David de Gea leaves Spain training on Friday to get a dislocated finger looked at
    Kipa namba moja wa Man United, David de Gea aliumia mazoezini na timu yake ya taifa, Hispania
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YAKABILIWA NA TATIZO LA KIPA KUELEKEA MECHI NA ARSENAL JUMAMOSI EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top