• HABARI MPYA

    Saturday, November 01, 2014

    DE GEA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MAN UNITED KWA ASILIMIA 70

    MASHABIKI wa Manchester United wamemchagua kipa David de Gea kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa klabu hiyo, baada ya Mspanyola huyo kupata asilimia 70 ya jura zilizopigwa kwenye mtandao.
    Licha ya kushindwa kuzuia nyavu zake kutikiswa katika mchezo wowote mwezi huo, De Gea alikuwa katika kiwango kizuri wakati United ikiifunga Everton kabla ya kutoa sare na West Brom ugenini na baadaye na vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea nyumbani.
    Mlinda mango huyo mwenye umri wa miaka 23 alipangua mkwaju wa penalti Leighton Baines na kuokoa michomo miwili ya hatari ya The Toffees dakika za mwishoni, kuiwezesha timu ya Old Trafford kupata pointi moja, kabla ya kuokoa mchomo mwingine wa Eden Hazard wakati Mbelgiji hjuyo alipopata nafasi nzuri ya kufunga timu hiyo ikitoka 1-1 na kikosi cha Jose Mourinho. 
    Kipa David de Gea akiwa amepozi na tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Oktoba Manchester United 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DE GEA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MAN UNITED KWA ASILIMIA 70 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top