// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YAW BERKO ASAINI MWAKA MMOJA LIBERTY PROF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YAW BERKO ASAINI MWAKA MMOJA LIBERTY PROF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, August 12, 2014

    YAW BERKO ASAINI MWAKA MMOJA LIBERTY PROF

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    ALIYEKUWA kipa wa Simba SC, Yaw Berko amejiunga na klabu yake ya zamani, Liberty Professionals FC y Ghana.
    Berko ameiambia BIN ZUBEIRY kwa simu jana kwamba amesaini Mkataba wa mwaka mmoja na Liberty baada ya kumaliza Mkataba wake wa miezi sita Simba SC.
    Berko alisajiliwa Desemba mwaka jana Simba SC kama mchezaji huru baada ya kutemwa na Yanga SC msimu wa 2012/2013, hata hivyo akadaka mechi tano tu na kufungwa mabao sita kutokana na kuzidiwa kete na Ivo Mapunda, aliyekuwa kipa namba moja.
    Yaw Berko amerejea Liberty Proffessionals ya Ghana

    Alidaka Simba SC ikishinda 3-1 dhidi ya KMKM mchezo wa kirafiki, Dar es Salaam akafungwa bao moja, akadaka Simba SC ikishinda 1-0 na KMKM tena, akadaka Simba SC ikifungwa 1-0 na Mtibwa Sugar mchezo wa kirafiki, akafungwa moja, akadaka Simba SC ikitoka sare ya 1-1 na Mbeya City mchezo wa Ligi Kuu mjini Mbeya akafungwa moja kabla ya kudaka Simba SC ikifungwa 3-2 na JKT Ruvu Ligi Kuu akafungwa zote tatu.
    Simba SC haikumuongezea mkataba mwishoni mwa msimu na sasa amerejea timu iliyomlea kisoka, Liberty.
    Berko alianzia soka Liberty Professionals FC na mwaka 2005 alikwenda kucheza kwa mkopo Pisico Binh Dịnh FC ya Vietnam kabla ya kurejea Ghana baada ya mwaka mmoja. Alijiunga na Yanga SC Desemba mwaka 2009 na kucheza hadi 2013.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YAW BERKO ASAINI MWAKA MMOJA LIBERTY PROF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top