• HABARI MPYA

    Tuesday, August 12, 2014

    KMKM CHUPUCHUPU KWA ADAMMA KAGAME, YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO

    BAO la Juma Mbwana Fakhi dakika ya 90 na ushei, limeinusuru KMKM kuzama mbele ya Adamma, baada ya kulazimisha sare ya 1-1 katika mchezo wa Kundi A, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Uwanja wa Nyamirambo, Kigali, Rwanda.
    KMKM baada ya kusawazisha bao leo Nyamirambo

    Adamma ya Ethiopia ilitangulia kupata kipindi cha pili mfungaji Wonooson Milkesa kabla ya KMKM ya Zanzibar kukomboa dakika za majeruhi.
    Hiyo ni sare ya pili kwa KMKM baada ya awali kutoka 1-1 pia Atlabara uya Sudan Kusini kabla ya kufungwa 4-0 na Azam FC, wakati Adamma katika mchezo wake wa kwanza ilifungwa 2-1 na Rayon.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KMKM CHUPUCHUPU KWA ADAMMA KAGAME, YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top